YAMENIKUTA JAMANI KUTONGOZA FACEBOOK SO INSHU




Ilikuwa Tarehe 26 - 06 Mwaka Huu Nilimuona Msichana Mrembo Facebook Basi Nikampenda Buree, Nikamwendea Messenger Kumwambia Ukweli wangu.
Nilipofika Messenger Nikamweleza Ukweli wangu na Kumwambia Ninapoishi. Mungu mkubwa Alinielewa na Kukubali Kuwa na Mahusiano nae. Aliniambia Anaishi Moshi namimi Nilikuwa Sumbawanga.
Tukapeana Appointment Tarehe 28 Tukutane Tabora stand Ili Tukafanye yetu. Nilisafiri kwa Gharama zangu naye Nilimtumia Hela ya Usafiri Tsh. 250,000 Kwa Bahatu nzuri Tukakutana Kweli..... Ilikuwa ni Furaha sana kwetu. Kiukweli Nilimuamini Sana na msichana Alikuwa Mzuri kama Nilivyo muona FB.
Bila kupoteza Muda Tukaenda Katika Hotel moja ya Kisasa Tukapata Vinywaji kwa Pesa yangu kisha Tukaenda Chumbani.
Ile Tunapanda Kitandani Alisita sita Kupanda kwa Uoga Basi minikajua Bikra Kumbe Lina Vunga tu hamna lolote.
Alipanda Baada ya Kumbembeleza Basi Tukafanya yetu. Huku pembeni kuna Bia 3 Aina ya Serengeti na Glass 2.
Nakumbuka kabla Hatujaanza Kufanya mapenzi Alininywesha Bia Basi nami Nikalewa Haswaa.
Nilipoteza Network Kwa Muda Nilikuwa Naona Ukungu Mbele yangu Sijui kama Tulifanya ama la!
Ile Nakuja Kushtuka Baada ya Muda najikuta Niko Pekeangu Niko Uchi , Pesa Hakuna na Mwanamke yule Hayupo.
Nikahitaji kwenda kuuliza Kwa Wahudumu lakini Nilikuwa Uchi na Hamna Nguo yoyote hata Taulo.
Daaah! Jasho lilinitoka Bila Formula Ila nacho mshukuru Mungu Simu yangu Tecno L8 Hakuiona Sijui Maana Nilikuwa nayo.
Nilikuwa na Akiba M-Pesa Hivyo nilimtuma Muhudumu akanitolee kisha Akaninunulie nguo Maana Alikuwa wa Kiume ko Tulielewana Hadi chumbani Alikuwa Akiingia.
Muhudumu Alinifanyia yote..... Nacho mdhukuru Mungu Sijafa basi!
Hadi sasahivi nipo Hapa Gest Nampango wa Kuondoka Kesho Asubuhi kwenda Sumbawanga kwangu.
Wallah Nimekoma Mademu wa Facebook ni Wezi maanaa kwa Haraka kabla hatujalala Nilikuwa na Tsh. 3,200,500 Kaiba zote!
Jamani Kama Umenielewa Shusha comment yako Kisha Share Ili Vijana Wajifunze!

Comments